Idadi Na Majina Wa Watoto Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

SWALI:

ASALAM ALYKUM MIMI NAULIZA MTUME MUHAMMAD(S.A.W), KAZAA WATOTO WANGAPI NA
KWA MKE YUPI NAYUPI,NA MAJINA
YAO HAO WATOTO NI NANI NA NANI SAMAHANI KWA USUMBUFU.

 


 

JIBU:

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Idadi ya watoto wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni saba; watatu wa kiume na wanne wa kike nao ni:

Wa kiume :  Al-Qaasim, 'Abdullaah   na Ibraahiym.

Wanawake: Zaynab, Ruqayyah, Ummu Kulthuum na Faatwimah.

Watoto wote amezaa nao kwa Bibi Khadija Bint Khuwaylid رضي الله عنها  isipokuwa Ibraahiym amezaa na Maria Al- Qibtwiyah (Radhiya Allahu 'anhaa)

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share