Bajia Laini Za Kunde

Bajia Laini Za Kunde

Vipimo

Kunde za kupaazwa - 2 gilasi

Vitunguu - 4 au 5

Pilipili boga tamu la kijani (capsicum) - 1 kubwa

Pilipili mbichi kijani - 2 - 3

Chumvi  - kiasi

Kotmiri katakata (coriander) - 1 msongo (bunch)

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chagua kunde toa vijiwe, osha kisha roweka kwa muda wa masaa 3 au zaidi.
  2. Katakata vitunguu mapande makubwa kubwa kiasi na pia pilipili tamu kubwa.
  3. Zichuje kunde maji, kisha tia katika mashine ya kusagia (blender) kiasi kidogo cha kunde, vitunguu, pilipili boga, pilipili mbichi na weka maji kiasi cha kuwezesha kusagika tu kunde.
  4. Saga vizuri, kisha chuja. Weka kunde ulizosaga katika bakuli kubwa.
  5. Tumia maji uliyoyachuja kusagia kunde zilobakia kwa kiasi kidogo kidogo mpaka zimalizike.
  6. Changanya vizuri mchanganyiko katika bakuli na weka kotmiri na chumvi uchanganye vizuri tena.
  7. Weka mafuta katika karai, teka mteko mdogo mdogo wa duara uchome bajia katika mafuta ya moto.
  8. Zikigeuka rangi kuwa za hudhurungi (golden brown), epua chuja mafuta zikiwa tayari kuliwa na chatine ya nazi. 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share