Skip navigation.
Home kabah

Hukmu Ya Kusherehekea Mawlid Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

Hukmu Ya Kusherehekea Mawlid Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Katika Mwezi Wa Rabiy’ul-Awwal Kwa Ajili Ya Kumuadhimisha

 

Al-Lajnah Ad-Daa'imah

www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kusherehekea mawlid ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika mwezi wa Rabiy’ul Awwal kwa ajili ya kumuadhimisha?

 

 

JIBU:

 

Kumuadhimisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumheshimu ni kwa  kuamini kila alilokuja nalo kutoka kwa Allaah, na kufuata Shariy’ah Yake, ki-‘Aqiydah, na kwa kauli na kwa matendo na tabia, na kuacha bid’ah katika Dini.

Na katika mambo ya bid’ah ni kusherehekea Mawlid Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Wa biLLaahit-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fatwa (3257) – Al-Lajnah Ad-Daaimah]

 

 

 

Rudi Juu