Kuhusisha Siku Ya Mawlid Kwa Kuielezea
Siyrah Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Shaykh Swaalih Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Mimi ni Imaam wa Masjid, nimeombwa na wanaoswali niwasomee Siyrah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Jumatatu ijayo tarehe 12 Rabiy’ul Awwal.
JIBU:
Hapana! Usiwasomee! Usiwasomee siku ya Jumatatu kamwe kwa sababu hiyo ni kwa ajili ya Jumatatu ambayo ni sawa na tarehe 12 Rabiy’ul Awwal, jambo ambalo ni bid’ah. Hivyo usiwasomee wala usiwaitike.
[Mawqi' Ar-Rasmiy li-Ma'aaliy Shaykh Swaalih bin Fawzaan]