Keki Ya Tende Ya Mdalasini

Keki Ya Tende Ya  Mdalasini

Vipimo 

Unga  -  5 ½ vikombe

Tende (toa kokwa na katatkata)  -  2 ½ vikombe

Mayai -  10

Siagi -  400 gms

Sukari ilosagwa -  3 vikombe

Baking powder - 3 vijiko vya chai

Bicarbonate soda - 1 kijiko cha chai

Maziwa ya unga -  3 vijiko vya kulia

Mtindi (yoghurt) -  1 kikombe                

Mafuta - ¼ kikombe

Vanilla -  1 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga -  1 kijiko cha chai

Hiliki -  ½ kijiko cha chai

Chumvi  - ½ kijiko cha chai                                   

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni mapema kiasi.
  2. Roweka  tende katika kibakuli kwa kutia maji ya moto ya kuchemka kiasi vikombe 2 vya maji.  Changanya na bicarbonate soda kuilainisha. Roweka dakika chache.
  3. Changanya na mtindi, upige vizuri mpaka mchanganyiko uwe nyororo.
  4. Katika  bakuli jengine, changanya siagi, mafuta, sukari pamoja upige kwa mashine au kwa mkono mpaka iwe creamy na nyeupe.
  5. Tia mayai uliyoyapiga pembeni uchanganye pamoja na vanilla, mdalasini na hiliki.
  6. Tia mchanganyiko wa tende ukoroge ichaganyike.
  7. Tia unga kidogokidogo huku ukichaganya na baking powder. Kisha tia maziwa uchaganye.
  8. Mimina katika treya ya  kuokea katika oven (baking trayer) uoke (bake) katika oen kiasi moto wa 360 Degrees kwa muda wa ½ saa  takriban.  Hakikisha imewiva. Epua ikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Kidokezo:  Unaweza kutoa keki mbili kutegemea na saizi ya treya unazotumia.

 

 

 

Share