Vikeki Vidogo Vya Chenga Za Shayiri

 Vikeki Vidogo Vya Chenga Za Shayiri 
 

Vipimo

Unga - 2 Vikombe

Chenga za shayiri (oatmeal) - 1Kikombe

Baking Powder - 1 Kijiko Cha Supu

Baking Soda - ½Kijiko Cha Chai

Chumvi -  ½Kijiko Cha Chai

Sukari Ya Buni - 1 Kikombe

(Brown Sugar)

Mdalasini - 1 Kijiko Cha Chai

Mayai -  2

Mafuta -  ½Kikombe

Mtindi (yogurt) -  1½ Vikombe

Vanilla -  1 Kijiko Cha Chai

Karoti Ziliokunwa(grated) - 1 Kikombe(Karoti 3) 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Chunga  pamoja unga,  oatmeal,  baking powder, baking soda, chumvi, sukari ya buni, mdalasini.
  2. Changanya mayai, mafuta, mtindi na vanilla kwenye bakuli.Tia karoti kisha ule mchanganyiko wa unga.
  3. Chota mchanganyiko kwa kijiko tia ndani ya treya maalum ya kupikia muffins/cupcakes.
  4. Pika (bake) katika oveni lenye moto wa 350º F kwa dakika 30.

 

Share