Keki Ya Semolina Na Jozi (Walnut)
Vipimo
Mayai 5
Sukari 2 Vikombe vya chai
Mafuta 2 Vikombe vya chai
Maziwa 2 Vikombe vya chai
Semolina 2 vikombe vya chai
Baking powder 3 Vijiko vya chai
Jozi zilizosagwa (Walnuts) 4 Vikombe vya chai
Ganda la ndimu iliyokaruzwa 1
Unga ½ kuzidi kidogo kikombe cha chai
Shira
Sukari 4 Vikombe vya chai
Mai 4 Vikombe vya chai
Ndimu 3 Slesi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Washa oveni moto wa 300F.
2. Kwenye bakuli kubwa, changanya vizuri vipimo vyote pamoja isipokuwa kikombe kimoja cha jozi (walnuts), ya kunyunyizia juu kupambia.
3. Mimina mchanganyiko kwenye chombo cha kuvumbika.
4. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 45 au zaidi hadi iwive.
5. Ipike shira kwa kuiacha ichemke dakika chache tu.
6. Kisha mimina juu ya keki iliyokwishaiva, na unyunyizie ile jozi iliyobaki
7. Iache ipoe kabisa kabla ya kuandaa.
Kidokezo: Inapendeza kuliwa ikiwa baridi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


