196-Asbaabun-Nuzuwul: Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. Na kama mkizuilika….

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 196: Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.  Na kama mkizuilika…

 

 

 وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾

196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.  Na kama mkizuilika basi chinjeni wanyama walio wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam au kutoa swadaqah au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye kujistarehesha kwa kutekeleza ‘Umrah kwanza kisha Hajj, achinje mnyama aliye mwepesi. Na asiyepata afunge Swiyaam siku tatu katika Hajj na saba mtakaporejea. Hizo ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Al-Masjidil-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Mkali wa kuakibu.

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عن صفوان بن يعلى بن أمية عن أبيه قال: جاء إلى رسول صلى الله عليه وعلى آله وسلم وقال: كيف تأمرني في عمرتي، فأنزل الله عز وجل : ((وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّهِ)) فقال رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم: ((من السائل عن العمرة)) فقال: أنا. فقال:((ألق ثيابك واغتسل واستنشق ما استطعت وما كنت صانعا في حجتك فاصنع في عمرتك))

Imepokelewa kutoka kwa Swafwaan bin Ya’laa bin Umayyah kutoka kwa baba yake kwamba: Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Unaniamrishaje kuhusu ‘Umrah yangu? Hapo Allaah (عز وجلَّ)  Akateremsha: “Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.”. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nani aliyeuliza kuhusu ‘Umrah?”  Akajibu: Mimi. Akasema: “Toa nguo zako, uoge, usukutue uwezavyo na fanya katika ‘Umrah yako kama ulivyokuwa ukifanya katika Hajj yako.” [Atw-Twabaraaniy].

 

Na kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake….” mpaka mwisho wake, imeteremka kuhusu Swahaba Ka’ab Ibn ‘Ujrah kama alivyohadithia kwamba: 

رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَقَفَ عَلَيْهِ وَرَأْسُهُ يَتَهَافَتُ قَمْلاً فَقَالَ: ((أَيُؤْذِيكَ هَوَامُّكَ))‏.‏ قُلْتُ نَعَمْ.‏ قَالَ: ((‏فَاحْلِقْ رَأْسَكَ)) قَالَ فَفِيَّ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِنْ رَأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِنْ صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ)) ‏فَقَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((صُمْ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ أَوْ تَصَدَّقْ بِفَرَقٍ بَيْنَ سِتَّةِ مَسَاكِينَ أَوِ انْسُكْ مَا تَيَسَّرَ))‏

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama karibu yangu, na chawa walikuwa wakianguka kutoka kichwani mwangu. Akasema: “Je chawa wanakutatiza?” Nikasema Ndio. Akaniamrisha kichwa kinyolewe. Ka’ab Akasema: Aayah hii imeteremshwa kunihusu mimi. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam au kutoa swadaqah au kuchinja mnyama…” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniamrisha nifunge Swawm siku tatu au kulisha masikini sita kwa faraq (Nusu ya pishi za tende au  chakula kinginecho kwa kila maskini mmoja; jumla ni pishi tatu kwa maskini sita) au kuchinja kafara, kondoo au kilichopatikana wepesi. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Ka’b (رضي الله عنه)].

 

 

Share