197-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 197: وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 197:  Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji ...

 

 

الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

197. Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya khayr Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!

 

 

Sababun-Nuzuwl:  

 

Sababu ya kuteremka Kauli ya Allaah: “Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa.” Watu wa Yemen walikuwa wanapokwenda Hajj hawachukui matumizi ya njiani na khatimae wanasema: “Sisi ni wenye kutawakali kwa Allaah.” Na wakiingia Makkah, wanaanza kuombaomba watu. Hapo ikateremka Aayah. [Al-Bukhaariy kutoka kwa ‘Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]  

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ:  كَانَ أَهْلُ الْيَمَنِ يَحُجُّونَ وَلاَ يَتَزَوَّدُونَ وَيَقُولُونَ نَحْنُ الْمُتَوَكِّلُونَ، فَإِذَا قَدِمُوا مَكَّةَ سَأَلُوا النَّاسَ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: ((‏وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى‏))

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba: Watu wa Yemen walikuwa wanapokwenda Hajj hawachukui matumizi ya njiani na khatimae wanasema: “Sisi ni wenye kutawakali kwa Allaah.” Na wakiingia Makkah, wanaanza kuombaomba watu.  Allaah تعالى Akateremsha: Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa.” [Al-Bukhaariy katika Kitaab Al-Hajj, na Sunan Abiy Daawuwd Kitaab Al-Manaasik]

 

Miezi ya Hajj:

 

Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amesema: “Miezi ya Hajj ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)]

 

 

 

 

 

 

 

Share