Imaam Ibn Baaz: Maana Ya "Allaah Ni Nuru Ya Mbingu Na Ardhi"

Maana Ya "Allaah Ni Nuru Ya Mbingu Na Ardhi"

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Nataka kujua Tafsiyr ya kauli Yake (Ta’aalaa):

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ  

Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi.  [An-Nuwr: 35]

 

 

Jibu:

 

 

Maana ya Aayah hiyo tukufu  kwa maelezo ya ‘Ulamaa ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amezinawirisha. Kwa hiyo, nuru yote iliyoko mbinguni na ardhini na Siku ya Qiyaamah, yote ni kutokana na Nuru Yake (Subhaanahu wa Ta'aalaa). 

 

Na Nuru ni aina mbili:

 

Nuru ya kwanza: Iliyoumbwa ambayo inapatikana duniani na Aakhirah na Jannah, na baina ya watu hivi sasa, nazo ni ambazo zinatokana na mwezi, na jua na nyota, na kadhaalika kama mwanga wa umeme na moto, zote hizo zimeumbwa na ni miongoni mwa viumbe Vyake (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Nuru ya pili: Ni ambayo haikuumbwa bali ni katika Sifa Zake (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na Allaah (Subhaanahu wa bi-Hamdihi) kwa Sifa Zake zote, Yeye ni Muumba na asiyekuwa yeye inakuwa ni kiumbe. 

 

Kwa hiyo, Nuru ya Wajihi Wake (‘Azza wa Jalla) na Nuru ya dhati Yake (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zote hizo hazikuumbwa bali ni Sifa katika Sifa Zake (Jalla wa ‘Alaa). Na hiyo ndio Nuru ‘Adhimu Aliyeisifia (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ambayo haikuumbwa bali ni katika Sifa Zake, kama vile Sifa za kusikia Kwake, na kuona Kwake, na Mkono Wake, na Mguu Wake, na kadhaalika katika Sifa Zake ‘Adhimu (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na hii ndiyo haki kama waliosimama juu yake  Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah.

 

 

[http://www.binbaz.org.sa/fatawa/247]

 

 

 

 

Share