Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kujilazimisha Kutoa Swadaqah Kwa Kuona Hayaa

 

Kujilazimisha Kutoa Swadaqah Kwa Kuona Hayaa

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nilitoa pesa kazini kwa ajili ya jambo la manufaa, lakini nilitoa kwa sababu tu ya kuona hayaa mbele ya  bosi wangu. Ingelikuwa ni katika uwezo wangu, nisingelitoa hata nusu ya riyali. Je nitalipwa thawabu kwa kutoa kama vile nimetoa kwa moyo wa kuridhika?  Tafadhali nipe jibu kwa dalili.

 

 

JIBU:

 

Ikiwa hali ya jambo hilo nii kama ulivyoelezea, basi kutoa kwako swadaqah hiyo hutolipwa thawabu kwa sababu hukutilia niyyah kupata radhi za Allaah, bali umetoa kwa ajili ya Mwajiri wako kwa sababu ya kumwogopa au kuona hayaa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى  

((Hakika (kusihi kwa) ‘amali kunategemea niyyah, na kila mtu atapata (malipo) kwa mujibu wa kile alichokinuia))

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah – Fataawa Islaamiyyah (8/104)]

 

 

Share