Crapes Kwa Maple Syrup Ya Canada

Crapes Kwa  Maple Syrup Ya Canada

 

 

Vipimo 

Unga mweupe -1 ½ kikombe

Baking powder- 1 kijiko cha chai

Baking soda- 1 kijiko cha chai

Yai- 1

Sukari -3 vijiko vya kulia

Maziwa -1 kikombe

Siagi (butter)- vijiko 2 vya kulia

Mafuta -1 kijiko cha kulia

Vanilla- 2 vijiko vya chai

Chumvi - ¼ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka unga, sukari, baking powder, baking soda na humvi katika bakuli kubwa.
  2. Tia maziwa, yai, siagi, vanila na vilobakia   
  3. Piga kwa mchapo (Whisk) vichanganyike vizuri
  4. Weka kikaangio (fyring pan) kisichoganda katika moto wa kiasi.
  5. Pakaza chuma mafuta au samli kisha mimina mchoto wa kiasi upendacho. Tandaza upikike hadi utoe vitundu (bubbles) na ugeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
  6. Geuze upande wa pili ukipikika epua uweke kwenye sahani.
  7. Tolea kwa canadian maple syrup (au asali ukikosa)

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share