Halawiyaat Fatwaair Bil-Jibnah (Vitobosho Vitamu Kwa Jibini)

Halawiyaat Fatwaair Bil-Jibnah  (Vitobosho Vitamu Kwa Jibini)

 

 

Vipimo:

Manda za sambusa za tayari - *idadi unayotaka

Jibini (cheese) ya vipande

(Ikiwa ni kiri kata kipande kimoja cha jibini katika vipande 5)

Lozi na pistachio zilizosagwa - 1 Kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kata kata jibini vipande vidogo
  2. Tia kipande kimoja cha jibini katika manda na  uifunike kwa kuizungusha manda hadi mwisho iwe katika umbo la mstatili (kama katika picha)
  3. Funga mwishoni kwa gundi ya unga kama unavyofunga sambusa.
  4. Kaanga katika mafuta kama unavyokaanga sambusa.
  5. Epua kwenye mafuta na tia katika shira kisha zitoe na zipange katika sahani.
  6. Saga lozi (na pistachio kama unazo) kama unga kisha nyunyizia juu yake.

 

Shira:

 

Sukari - 1 Kikombe

Maji - 3/4 Kikombe

Zaafarani rowanisha - 1 kijiko cha chai

Ipikie shira pamoja na zaafarani hadi iwe tayari, isiwe nzito  

 

*Kidokezo:

 

Wingi wa Halawiyaat Fatwaair Bil-Jibnah zinategemea manda za sambusa na kiasi unachotaka mwenyewe, hivyo kila manda moja ya sambusa utie kipande kimoja cha jibini.

 

 

Share