050-Aayah Na Mafunzo: Watu Watatu Wenye Kuchukiza Zaidi Kwa Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Maaidah

Watu Watatu Wenye Kuchukiza Zaidi Kwa Allaah

 

 

 أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

50. Je, wanataka hukumu ya (enzi ya) ujahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.

 

Mafunzo:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu wenye kuchukiza zaidi kwa Allaah ni; Mweye kufanya uovu katika Al-Haram (Makkah), mwenye kutafuta katika Uislamu mwenendo wa jaahiliyyah, (enzi za ujinga kabla ya Uislamu) na mwenye kutafuta damu ya mtu ili aimwage bila ya haki.” [Al-Bukhaariy].

 

 

 

Share