256-Asbaabun-Nuzuwul: Hapana kulazimisha katika Dini...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 256: Hapana kulazimisha katika Dini

 

 لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾

256. Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaghuti na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii: “Hapana kulazimisha katika Dini…” imeteremka kuhusu mwanamke ambaye alikuwa kila anapozaa mtoto wake hufariki. Basi mwanamke huyo akaweka nadhiri katika nafsi yake kwamba pindi akizaa na akaishi mtoto wake asife, atamfanya kuwa Yahudi. Na walipotolewa Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr, kulikuwa katika wao kuna watoto wa Answaar. Kisha wakasema: “Hatuwaachi watoto wetu!” (Wakikusudia na mtoto huyo?)  Hapo ikateremeka Aayah hii [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]   

 

 

 

 

Share