Cookies Za Tende Na Tangawizi

Cookies Za Tende Na Tangawizi

 

 

Vipimo 

 

Unga vikombe vikombe 4

Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto

Siagi 400 gms

Sukari ½  kikombe

Tende chambua ukatekate ifikie ¾ kikombe

Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai

Vanilla 1 kijiko cha chai

Yai 1

Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo.
  2. Tia yai uchanganye vizuri
  3. Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri.
  4. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko).
  5. Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive.
  6. Epua vikiwa tayari

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share