Swalaah Za Sunnah Zilizo Sahihi Na Ambazo Si Sahihi

 

 Swalaah Za Sunnah Zilizo Sahihi Na Ambazo Si Sahihi

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalaamualaykum   ndugu   zangu,

Mimi siku zote   naamka saa nane  za usiku,  yaani na amshwa naturally. Nina sali kwa mpango   ufuatao:

 

1.      Sunnatil-udhuu       rakaa 2

2.      Sunnati    Rasulu-Allaah Swalla Allaahu alayhi wa sallam wa sallam rakaa   2

3.      Sunnat tahajjud    rakaa    2

4.      Sunna ya usiku ule  raka ....kama ilvyoandikwa

5.      Sunnat hajjat rakaa  2, 2,2,  mujibu wa haja  zangu.  

6.      Sunnat tawba    rakaa  2

7.      Salaatul  witr     rakaa   3.

 

By the time   nimewahi  zote   Swalah ya fajr   ni tayari.  na endelea  kufanya  dhikruAllaah  baada ya swalah  ya fajr   mpaka time ya   ishraaq    na tena   naendelea kuwepo  kwenye  msala kwa dhikru-Allaah mpaka   swalah ya dhuhaa.

Je    nifafanulieni   wapi nimekosea na  nifanye sahihi namna   gani

Jazaakallahukheir      

Fiamaanillah

 

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakika ‘ibaadah ni jambo muhimu sana kwa kila Muislamu kwani katika kufanya ‘ibaadah yoyote ikiwa ya vitendo au kauli,  lazima masharti mawili yapatikane ndipo ‘ibaadah hiyo ikubaliwe nayo ni:

 

 

1-Ikhlaas – Iwe kwa kutaka Radhi za  Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  na sio yenye Riyaa (kujionyesha) au sio yenye kutendeka kwa ajili ya maslahi ya kidunia.

 

2-Iwe inafanyika kutokana na mafunzo ya  Qur-aan na Sunnah.  

 

  

Tunakutajia hapa zilizo sahihi na zisizo sahihi kutokana na maelezo yako:

 

 

Swalaah

Daraja yake

Dalili/Maelezo

 

Sunnatul- Wudhuu  Rakaa mbili 

Sahihi

Bilaal (Radhwiya Allahu 'anhu) akiswali hata Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaota nyao zake ziko Jannah (Peponi) kwa kufanya hivyo

 

Sunnatul-Rasulu-Allaah    

Sio sahihi

Hakuna dalili yoyote.

 

 

Tahajjud Rakaa 2

Sahihi

 Ni Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku) Unaweza kuswali mbili, au nne, au sita au nane ukamalizia na tatu za Witr

 

 

Sunnah ya usiku

Sahih

Nayo ni Qiyaamul-Layl. Ni Swalaah yoyote unayoswali baada ya ‘Ishaa kama ni kisimamo cha usiku.

 

Sunnah ya Haja

Haifai

Imepingwa na ‘Ulamaa kuwa ni Hadiyth dhaifu. Muislamu anaomba haja zake kwa kuomba du'aa kama kawaida.

 

Sunnati Tawbah

Sahihi

Anapofanya mja dhambi anaswali Rakaa mbili kuomba maghfirah

Salaatul Witr

Sahihi

Rakaa 3 unamalizia baada ya kuswali 8 au chini yake za Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku)

Hii imesisitizwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Unavyomalizia kuwa inafika Alfajiri kisha unaendelea kufanya Dhikru-Allaah hadi litoke jua kisha unaswali Swalaah ya Dhwuhaa, hakika Hadiyth hiyo baadhi ya ‘Ulamaa wameona kuwa ni dhaifu na wengineo wameona kuwa ni sahihi. Nayo inatokana na Hadiyth ifuatayo:

   

 عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال : من صلى الفجر في جماعة ثم قعد يذكر الله  حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة تامة تامة  أخرج الترمذي  صححه الألباني

Imetoka kwa Anas kwamba   Nabiy   (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jamaa'ah kisha akakaa Anamdhukuru Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhy na kaisahihisha Al-Albaaniy] 

 

 

Kwa hiyo tekeleza ambazo ni sahihi na epukana na ambazo si sahihi au zina utata.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share