Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Tawassul Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Sehemu Tatu Inayojuzu Ni Moja Tu

 

Tawassul Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Imegawanyika Sehemu Tatu Inayojuzu Ni Moja Tu

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

“… Basi tunasema tawassul kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) imegawanyika sehemu tatu:

 

 

Kwanza: Atawassal mtu kwa iymaan yake kwake, na kwa kumfuata (Sunnah zake), na hii inakubalika katika uhai wake na baada ya kufariki kwake. (Mfano kusema: “Ee Allaah nakuomba kwa kutawassal kwa iymaan na mapenzi yangu kwa kufuata Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Unitakabalie kadhaa wa kadhaa.”   

 

 

Pili:  Atawassal kwa du’aa yake, yaani amwombe Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili amwombee mtu. Na hii inakubalika katika uhai wake wala si baada ya kufariki kwake, kwani baada ya kufariki kwake yeye ni mwenye udhuru (hayuko tena). 

 

 

Tatu:  Kutawassal kwa jaha yake na utukufu wake mbele ya Allaah. Hii haijuzu katika uhai wake wala si baada ya kufariki kwake, kwa sababu yeye siye wasiylah, hivyo hawezi kufikisha mtu katika lengo kwani si kazi yake.

 

Kwa hiyo akiuliza mtu: “Nimefika katika kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuomba anighufurie au anipe shafaa'ah (uombezi) mbele ya Allaah; je, inajuzu au haijuzu? Tunasema:  Haijuzu.”

 

 

[Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn - Hukmu At-Tawassul Wa Ahkaamuhu (2/25 -380)]

 

 

Share