Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kuweka Msahafu Kwa Ajili Ya Kutabarruk Na Kinga Ya Hasad Na Kijicho

 

Kuweka Msahafu Kwa Ajili Ya Kutabarruk Na Kinga Ya Hasad Na Kijicho

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kuweka Msahafu katika gari kwa ajili ya kutabarruk (kutafuta baraka) au kwa ajili ya kujikinga na kijicho na pia kukhofia ajali? Naomba jibu kutoka kwenu kuhusu hilo.

 

 

JIBU:

 

“Kuweka Msahafu katika gari kwa ajili ya kujikinga na kijicho au kujikinga na khatari (ajali) au kujikinga (kwa ujumla), ni bid’ah (na shirki).

Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) hawakuwa wakibeba Misahafu walipokuwa wakipanda ngamia wao kwa ajili ya kujikinga na khatari au jicho baya. Na hivyo basi kwa kuwa ni bid’ah, basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((Kila bid’ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni)).

 

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (2/4)]

 

 

Share