Skip navigation.
Home kabah

Keki ya maziwa

 

Vipimo

Siagi                                                               Kikombe 1

Sukari                                                             Kikombe 1 

Unga                                                               Vikombe 2 

Maziwa                                                           1/2 (nusu) Kikombe 

Mayai                                                              4

Baking Powder                                                1 Kijiko cha supu

Arki rose                                                           kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.                      Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.

2.         Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.

3.                       Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.

4.                       Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.

5.                       Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)

6.                       Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.

7.                       Ipike (Bake ) mpaka iwive.

8.        Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande. 

 

Assalamu Alaykum. Shukran

Assalamu Alaykum. Shukran sana kwa recipe hii. Mimi nina swali ndugu zangu. Sina oven nyumbani. Tafadhali nieleze, kama natumia jiko nitaitayarisha vipi keki hii?

A.alykum, Ningependa kuuliza

A.alykum,
Ningependa kuuliza kuwa vikombe vya kutumia ni vya chai au vikombe maalum vya kupimia?

Assalaamu álaykum Kwanza

Assalaamu álaykum

Kwanza tunapenda kukupa nasaha kutokufupisha maamkizi ya Kiislamu kwa kuandika (A. alaykum) n.k. kwani hivyo ni kukosa thawabu za fadhila zake na pia ni kinyume na mafunzo ya Dini yetu.

Ama kuhusu vipimo vya vikombe ni kuwa vilokusudiwa ni vikombe vya chai.

fiy amaaniLlaah

aha ntajaribu thn nita leta

aha ntajaribu thn nita leta matokeo thnx

assalam aleykum nimevutiwa

assalam aleykum nimevutiwa sana na website hii kwani inafundisha mambo yanayostahili inshallah allah atawazidishia kila la kheri na mafanikio ktk maisha ameen. unaweza kuchanganya bila mashine sasa utatumia kitu gani ktk kuchanganya baada ya mashine mana kama mie sina mashine ya keki.? na ukimaliza kuchanganya mchanganyiko wote unasubiri kwa muda au unaweka moja kwa moja kwenye oven? shukran sana

Mimi nafundisha na

Mimi nafundisha na kutengeneza cake za ocasion aina zote kuanzia birthday mpaka harusi.

Website yenu nzuri sana mapishi yake mashallah nimejaribu mojawapo na nina furaha kuwaambia vyakula vilitoka 100% vitamu.

shukran

Please explain in english

Please explain in english the ingridients used on cake icing and decoration.

asalam aleikum,

asalam aleikum,

samahani nilikuwa naomba kufahamishwa jinsi ya kutengeneza keki ya harusi na upambaji wake.

assalam alaykum I am one of

assalam alaykum

I am one of your member using this alhidaya website, I always try to use your recepe for different kind of foods. So I have one request can you please assist me on how to prepare icing sugar for the cake which i want to make on my daughers birthday end of this month? I will apreciate for doing so.

Thanks and may Allah bless you all.

wa 'alaykumus-salaam wa

wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLlaahi wa Barakaatuh

Tunashukuru kuwa unafaidika na mafunzo ya Alhidaaya. Lakini tunasikitika kuona kwamba umeomba jambo ambalo halipasi katika sheria (hukmu) ya Kiislamu. Hivyo inaonyesha kuwa hukupata bado mafunzo kuhusu hukmu ya kusheherekea siku ya kuzaliwa (Birthday). Jambo ambalo halipasi kwa Muislamu kwani hayo ni mambo ya kuiga makafiri. Na kuwaiga wao ni kujiingiza katika shirki na bid'a (uzushi) ulioharamishwa, hivyo nidhambi kubwa.

Ndugu yetu mpenzi, ni muhimu pia utembelee sehemu nyinginezo humu upate mafunzo ya Dini yako ambayo ni chakula cha moyo na ambacho ni muhimu zaidi. 

Tafadhali soma makala muhimu katika viungo vifuatavyo upate kujua hukmu yake na ubakie salama na Mola wako Mtukufu.

Historia Ya Keki Na Mishumaa Katika Kuadhimisha Siku Ya Kuzaliwa (Birthday)

Kusherehekea Siku Ya Kuzaliwa Inafaa?

Tunatumai kuwa utakuwa umepokea nasaha zetu za dhati kwako.

Ndugu zako

AL HIDAAYA 

Rudi Juu