Keki Ya Walnut (Jozi) Na Mdalasini

Keki Ya Walnut (Jozi) Na Mdalasini 

     

Vipimo: 

Unga  mweupe - 1 ½ kikombe 

Siagi - 10 vijiko vya supu  

Sukari ya brown (soft brown sugar)- ½ kikombe 

Baking powder -  1 ¾  kijiko cha chai  

Mayai -   2 

Maziwa -  ¼ kikombe

Walnut zilokatwakatwa (chopped) - 1 kikombe 

Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - ¼ kijiko cha chai 

Vanilla- ½ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Weka siagi nje iwe laini (katika room temperature) 
  2. Washa jiko la oveni kiasi cha 350° 
  3. Weka siagi katika bakuli ipige hadi iwe laini. 
  4. Tia mayai uendelee kupiga  
  5. Tia vitu vikavu vyote . 
  6. Tia maziwa kisha walnuts   
  7. Paka siagi katika treya ya kupikia keki iwe size ya kiasi inchi 8 au 9  
  8. Mimina mchanganyiko wa keki 
  9. Pika kwa muda wa dakika 35-40,  iangalie kama imeiva kwa kutia kijiti na kukitoa ikiwa kavu tayari, epua na iache ipoe.

 

 

 

 

Share