Sambusa Za Nyama

Sambusa Za Nyama

Vipimo

Manda ya sambusa ya tayari - Kiasi zinavyouzwa(Kiasi ya sambusa 40-50)

Mafuta ya kukaangia - Kiasi

Nyama ya Kusaga - 3LB (Pounds)

Kitunguu saumu(thomu) na tangawizi iliyosagwa - 2 Vijiko vha chai

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha supu

Garam masala - 1 kijiko cha supu

Chumvi - Kiasi

Vitunguu maji vilivyokatwa (chopped) - 3 Vidogo au 2  Vikubwa

Kotmiri iliyokatwa (chopped) - Kiasi

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Pika nyama ya kusagwa kwa kutia chumvi, thomu na tangawizi, pilipili na ndimu.
  2. Kabla haija kauka tia Garam masala.
  3. Zima moto acha kidogo ipoe tia vitunguu na kotimiri.
  4. Funga sambusa katika manda kama kawaida.
  5. Pika sambusa katika mafuta ya moto hadi ziwe nyekundu na zikiwa tayari kuliwa.

 

 

 

 

 

 

Share