Keki Za Vikombe Za Nazi (Coconut Muffins)

Keki Za Vikombe Za Nazi (Coconut Muffins)

Vipimo 

Unga-  ½ kikombe

Sukari -  ¼ kikombe

Siagi (margarine) - 1 kikombe

Mayai - 3

Baking powder - ½ kijicko cha chai

Maziwa mazito - kopo 1 (285ml)

Nazi (machicha) - 200 gms

Vanilla-  ½ kijiko cha chai teaspoon 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia kwenye bakuli siagi na sukari piga kwa mashine mpaka iwe laini kama malai (Cream)
  2. Tia mayai piga vizuri.
  3. Tia unga na baking powder.
  4. Tia nazi.
  5. Tia maziwa na vanilla, piga kidogo.
  6. Tumia treya za vishimo vya duara (muffin tray), weka karatasi zake, kisha tia mchanganyiko wa keki kiasi usijaze katika vishimo.
  7. Choma (bake) katika moto wa 325 C
  8. Choma kwa muda wa dakika 10 – 15 mpaka iwe rangi ya udongo kidogo (brown).
  9. Epua na tayari kwa kuliwa.
Share