Keki Ya Zabibu -2

Keki Ya Zabibu -2

Vipimo  

Siagi -  200g 

Unga -  2 Vikombe 

Sukari -  1 Kikombe 

Vanilla -  ½ Kijiko 

Arki rose ukipenda - 2 matone 

Mayai  - 6 

Zabibu -  ¼ Kikombe 

Baking powder - 2 Vijiko vya chai 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni 350°c.
  2. Saga siagi na sukari kwa mashine mpaka mchanganyiko ulainike.
  3. Ongeza yai moja baada ya moja na huku ukiendelea kusaga mpaka yaishe.
  4. Tia unga uliochanganwa na baking powder.
  5. Endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri, halafu arki rose, vanilla na zabibu halafu koroga kidogo ilizichanganyike vizuri.
  6. Mimina mchanganyiko katika chombo cha kuchomea.
  7. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 20 mpaka 25.
  8. Ikisha poa kata kata vipande na tayari kuliwa kwa kahawa au chai.
Share