Pai Ya Kuku (Chicken Pie)

Pai Ya Kuku (Chicken Pie)

Vipimo

Unga wa kitobosha (puff pastry) - 397-400 gm

Nyama ya kuku bila ya mifupa - ratili (LB)

Kabichi iliyokatwa nyembamba nyembamba Vikombe vya chai - 2               

Kitunguu saumu(thomu) na Tangawizi iliyosagwa -1 kijiko cha chakula

Chumvi - kiasi

Pili pili manga -1 kijiko cha chakula

Jirah (bizari ya pilau) - 1 kijiko cha chai

Mdalasini - 1 kijiko cha chai

Dania (corriander powder) - 1 kijiko cha chai

Ndimu au limau - 2 Vijiko vya chakula

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Kama unga  wa kitobosha (puff-pastry) uko katika barafu toa mapema kidogo.
  2. Washa jiko la oveni moto wa kiasi cha kiwango 375-400  Deg.
  3. Kata nyama ya kuku vipande vipande  kisha itie kwenye sufuria na tia ndani yake, thomu/tangawazi, chumvi, pilipili manga, jirah, mdalasini dania na ndimu.
  4. Mpike kuku kwa moto mdogo mdogo hadi awive. Akihitaji maji, tia kidogo tu kiasi cha kumpika awive asibakie na maji.
  5. Epua na chambua kuku. (Unaweze kutumia sehemu ya kuku ya mifupa, hivyo itabidi uchambue na kutoa mifupa pembeni).
  6. Sukuma unga wa kitobosha (puff-pastry). (Ukipenda kata madonge mawili zitokee pai mbili).
  7. Kuku atakuwa ameshapoa, mchanganye na kabichi vizuri ongeza vikolezo ukipenda kama chumvi, pilipili manga na ndimu.
  8. Weka mchanganyiko wa kuku na kabichi katikakati katika unga uliosukuma na kata kama miba ya samaki (kama ilivyo katika picha)
  9. Suka kufunika vizuri kuku, huku unabana msuko ili ugandane.

     10. Ziweke pai katika trei ya oveni iliyopakwa siagi kidogo.

     11. Pika katika oven ambalo litakuwa tayari limeshashika moto unaohitajika. Pika hadi zigeuke rangi na ziwive.

    12. Epua, ziweke katika sahani ya kupakulia zikiwa tayari.                   

 

 

 

 

 

Share