Fatwaair Za Mjazo Wa Mchanganyiko

 

Fatwaair Za Mjazo Wa Mchanganyiko

 

 

 

Vipimo Vya Unga Wa Fatwaair

 

Unga - 4 Magi (au vikombe vya chai)

Maziwa ya maji - 1 ½ 

Maziwa ya unga – vijiko vya kulia

Sukari - 3 Vijiko vya kulia

Mafuta -Robo Magi

Mtindi – Vijiko 3 vya kulia

Hamira - 1 kijiko kikubwa cha kulia

Baking powder – 1 kijiko cha chai

Chumvi - robo kijiko cha chai

 

 

Namna Ya Kutayarisha Mchanganyiko Wa Fatwaair

 

Tia katika mashine vitu vyote isipokuwa unga upige vichanganyike vizuri.

Tia unga kidogo kidogo huku unachanganya mpaka umalizike.

Ukishachanganyika unga wote, utazame usiwe wenye kunata sana, ikiwa unanata sana ongezea kidogo unga.

Utoe katika mashine na uweke katika bakuli ufunike kwa muda mpaka ufure.

Katakata vidonge vidogo dogo usukume, na ukate shepu upendavyo na ujaze michanganyiko utakayo kama kuku, nyama, sausage, saladi ya mayonnaise, zaatari, sosi ya pizza, samaki na kadhaalika.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Kidokezo:

 

Unaweza kupata aina ya mijazo katika viungo vifuatavyo:

 

Pai Ya Kuku (Chicken Pie)

 

Pai Za Kuku Na Kabichi

Sandwichi Za Soseji

Sandwichi Ya Samaki Tuna Mayonaise Na Jibini Ya Mazorella

Burger Ya Samaki Tuna

Samaki Wa Tuna Katika Mzungurisho Wa Mkate Wa Pita-Pan

Quesadilla (Kay-sa-dee-yya) Ya Kuku Na Uyoga (Spanish)

Quesadilla (Kay-sa-dee-yya) Ya Kuku, Pilipili Boga Na Vitunguu (Spanish)

 

 

 

 

Share