Supu-Uji
Supu Ya Mchanganyiko Wa Adesi Za Nazi Kwa Celery Karoti Viazi Mchicha

Vipimo
Machanganyiko wa adesi za kijani, nyekundu, brown - vikombe 2
Celery – mche mmoja
Karoti - 1
Viazi - 2
Bizari njano ½ kijiko
Jira (cumin, bizarii ya pilau) 1 kijiko cha chai
Paprika – 1 kijiko cha chai
Gilgilani (coriander) - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi- 2 vijiko vya chai
Nyanya kopo – vijiko 2 vya supu
Tui la nazi – vikombe 2
Mchicha – vikombe 3
Supu yoyote upendayo
Mafuta - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na kupika
- Weka mafuta katika sufuria tia vitunguu, kaanga kidogo kisha tia celery, karoti na viazi kaanga kidogo.
- Tia bizari zote, chumvi, tia maji kidogo.
- Tia adesi zote, kisha tia supu ya kutosha koroga.
- Tia nyanya kopo kisha acha ipikike viive vitu vyote na kuwa nzito kidogo.
- Tia tui la nazi (ukipenda), tia mchicha koroga kidogo tu ili mchicha usipikike sana.
- Epua ikiwa tayari.
- Unapopakua katika vibakuli tia juu yake mtindi kiasi vijiko viwili, nyunyizia kotmiri, pilipili mbichi zilokatwakatwa (ukipenda) na kitunguu kilokatwakatwa kwa ajili ya kupambia na kuzidisha ladha.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)