Supu Ya Kuku Ya Mboga Na Sosi Ya Beshamel

Supu Ya Kuku Ya Mboga Na Sosi Ya Beshamel

Vipimo

Kuku - ½

Chumvi - kiasi

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Kiazi - 1

Kiazi kitamu - 1

Brokoli - kipande kiasi

Koliflower (cauliflower) - kipande kiasi

Karoti - 2

Boga - kipande kiasi

Mumunya - kipande kiasi

Uyoga (mushroom) - ½ kikombe

Mahindi machanga (baby corn) - kiasi

Parsely (aina ya kotmiri) - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na kupika 

  1. Muoshe kuku vizuri, toa ngozi, katakata, kisha weka katika sufuri, tia chumvi, pilipili manga na ndimu.
  2. Weka maji kiasi ya kutosha yasibakie mengi sana. Chemsha mpaka awive.
  3. Epua toa nyama kuku kisha toa mifupa, chambua chambua. Ukipenda bakisha mifupa.
  4. Katakata mboga zote vipande vipande na katakata (chop) parsley
  5. Weka mboga zote katika supu ya kuku zichemshe ziive kidogo tu.
  6. Rudisha nyama kuku ulochambua katika supu ichanganyike na mboga.
  7. Weka sufuria nyengine tengeneza beshamel.

Vipimo Vya Beshamel

Unga - 2 vijiko vya kulia

Siagi - 2 vijiko vya kulia

Maziwa  ya unga - 1 gilasi moja

Kidonge cha supu (stock) - 1

Namna ya kutengeneza Beshamel 

  1. Teka supu kiasi gilasi mbili changanya na maziwa.
  2. Weka siagi katika sufuria, tia unga kaanga mpaka uanze kugeuka rangi.
  3. Mimina maziwa, tia kidonge cha supu, kisha iache ichemke kiasi. 
  4. Mimina mchanganyiko wa kuku na mboga pamoja na supu kama imebakia kidogo. 
  5. Onja ukolezee kiasi upendavyo.
  6. Unaweza kupunguza uzito wa beshamel kwa kupunguza maziwa kidogo:

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share