Vitumbua Vya Kuku Vya Mboga Na Jibini (Cheese)

Vitumbua Vya Kuku Vya Mboga Na Jibini (Cheese)

 

Vipimo

 

Kidari cha kuku – kilo 1

Tangawizi na kitunguu thomu ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Paprika – 1 kijiko cha chai

Jira (bizari ya cumin) – 1 kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi – 1 kijiko cha chai

Kitunguu maji – 2 katakata

Karoti – 1 moja katakata nyembamba

Pilipili (capsicum) kubwa la kijani – kiasi katakata

Pilipili kubwa (capsicum) jekundu – kiasi katakata

Jibini (Cheese) ya cheddar – ilokunwa – kiasi

Mayai – 3 au 4

Baking powder – 1 ikijiko cha chai

Unga wa dengu – 1 kijko ukihitajika (ikiwa mchanganyiko umekuwa wa majimaji)

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kuchomea

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Chemsha kuku kwa bizari zote, tia chumvi, kitunguu thomu na tangawizi
  2. Weka katika machine la kukatia kidogodogo (Chopper) usage kiasi. Kama huna chopper tumia blender lakini usisage mpaka ikavurugika mno.
  3. Mimina katika bakuli.
  4. Tia vitunguu na mboga zote zilobakia  changanya vizuri
  5. Tia jibini (cheese)
  6. Piga mayai katika kibakuli kisha changanya.
  7. Tia baking powder. Ikiwa mchanganyiko umekuwa majimaji tia unga wa dengu kiasi changanya. Ikiwa mzito, ongezea yai.
  8. Weka chuma cha vitumbua uchome kama unavyopika vitumbua  

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share