Vibibi

Vibibi       

  

Vipimo

Mchele - 2 Vikombe

Tui la nazi -  1 1/2 Kikombe

Mafuta - 1 kijiko cha supu

Hamira - 2 Vijiko vya chai

Unga wa ngano - 1 kijiko cha supu

Hiliki - kiasi upendavyo

Sukari  - ¾ au 1 Kikombe

Namna Ya Kupika Na Kutayarisha

  1. Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
  2. Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
  3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
  4. Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri ; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
  5. Weka chuma kipate moto.
  6. Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
  7. Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
  8. Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.

Kidokezo
Unaweza kutumia chuma kisichoganda ( non stick ) ; nacho hakitaraji kutiwa mafuta.

 

 

 
 
Share