Maandazi Ya Kusuka Ya Kunyunyuzia Sukari, Karameli, Chokoleti

 

Maandazi Ya Kusuka Ya Kunyunyuzia Sukari, Karameli, Chokoleti

 

 

Vipimo

 

 

Unga mweupe – vikombe 6

Sukari – vijiko 2 vya kulia

Hamira  ya instant  vijiko 2 vya kulia

Samli – kijiko 1 cha kulia

Mtindi – vijiko 2 vya kulia

Tui la nazi 2 ½ vikombe takriban

Hiliki – 1 kijiko cha chai

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Changanya vitu pamoja katika bakuli la kukandia unga. Au changanya vizuri kwa mkono kisha kanda vizuri.
  2. Utakapokuwa unga umechanganyika vizuri, utoe ufunike kiasi robo saa.
  3. Katakata vidonge usukume na kusuka na uweke katika treya.

  1. Yaache tena yaumuke vizuri.
  2. Kaanga katika mafuta yaliyoshika moto. Kaanga mpaka yageuke rangi kisha epua yachuje mafuta.
  3. Nyunyizia sukari laini nyororo (icing sugar) au karameli, au yayusha chokoleti, au shira au maziwa mazito na nyunyizia ufuta ukipenda.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Kidokezo:

 

Ukipenda tumia karameli zifuatazo:

 

Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito

 

Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream

 

 

 

 

Share