Kamba Wa Rojo

VIPIMO
Kamba (Prawns) Large size 1 Kg
Nyanya zilizosagwa (crushed) 3
Thomu na tangawizi 1 Kijiko cha soup
Nyanya ya mkebe (tomatoe paste) 1 kijiko cha soup
Pilipili kubwa (capsicum) (kata vipande vipande) 1
Pilipili mbichi 5- 6
Chumvi
Bizari ya pilau (cummin) powder ½ kijiko cha chai
Bizari ya giligilani (corriander ) powder ½ kijiko cha chai
Bizari ya manjano (Haldi) ½ Kijiko cha chai
Ndimu 1 Kijiko cha soup
Kotmiri (zilizokatwa ndogo ndogo ) ½ Kikombe
Mafuta ¼ Kikombe
NAMNA YA KUPIKA
1. Katika karai weka mafuta yapate moto, tia thomu na tangawizi.
2. Tia tomato zilizosagwa , kaanga, tia bizari zote endelea kukaanga .
3. Tia Pilipli kubwa, pilipili mbichi, chumvi, endelea kukaanga kidogo tu.
4. Tia Kamba, ndimu, kaanga, mwisho tia nyanya ya mkebe, endelea kukaanga

5. Mwisho kabisa mwagia kotmiri na pakua katika sahani.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


