Mishkaki Ya Nyama

Vipimo:
Nyama steki 4 Ratili (2 Kilo)
Mafuta 3 Vijiko vya supu
Masala Ya Kuroweka Katika Nyama:
Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Papai bichi kiasi lililochunwa ½ papai
Siki nyeupe 3 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Jiyrah (cummin powder/bizari ya pilau) 1 kijiko cha supu
Dania (coriander powder/gilgilani) 1 kijiko cha chai
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha supu
Mdalasini wa unga 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Kata nyama vipande vikubwa kubwa kiasi .
- Changanya masala na vitu vyote katika nyama uroweke kwa muda wa masaa mawili.
- Tunga vipande vya nyama katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers).
- Choma katika jiko la makaa au katika la B.B.Q kwa moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi nyama iwive.
- Epua, weka katika sahani ikiwa tayari kuliwa.
Kidokezo:
- Nzuri kuliwa na Hummus na mkate ya kiarabu (pita pan bread) – tazama pishi ya Hummus katika Saladi Na Sosi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


