Nyama Kuchoma Na Viazi

Vipimo
Nyama ya ng'ombe ya mafupa bila ya
kukatwa (pande kubwa) 5- 6 LB (au kiasi unachotaka)
Viazi vilivyomenywa na kukatwa duara 4 vikubwa
Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 Vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Mtindi (Yoghurt) 1 Kijiko cha supu
Pilipili manga ya unga 2 vijiko vya chai
Bizari ya pilau ya unga
(Jiyra/cummin powder) 2 vijiko vya chai
Siki 4 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya thomu, tangawizi, chumvi, pilipili manga, pilipili mbichi, mtindi, bizari ya pilau, na siki katika kibakuli kidogo.
2. Ichanje chanje nyama upate kuingiza mchanganyiko huo wa masala, kisha tia kidogo kidogo katika hizo sehemu wazi katika nyama na uroweke pande la nyama kwa muda wa nusu saa.
3. Liweke katika trea ya kupikia ndani ya jiko (oven). Ifunike kwa jaribosi ya kupikia (foil paper) na ipike katika moto mkali 400º- 450º kwa muda wa saa au zaidi. Inategemea ukubwa wa nyama, ikiwa ni pande kubwa
4. Karibu na kuwiva, vitie viazi chumvi na pilipili manga kidogo na umwagie juu ya nayma na uendelee kupika hadi viazi viwive pia.
5. Epua ikiwa tayari kuliwa.
Kidokezo: Nzuri kuliwa na mikate 'Pita pan bread, (au mikate ya kiarabu) saladi na hummus (sosi ya ufuta na dengu zilizosagwa). (Au sosi ya shawarma)
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


