Kuku Wa Tanduuri

VIPIMO
Kuku 5 pounds (vipande 20 – 25)
Ukwaju ½ pakti ( kwa kikombe kimoja cha maji)
Vitungu thaumu 1 kijiko kikubwa cha kulia
Tangawizi 1 kijiko kikubwa cha kulia
Uzile (binzari nyembamba ya unga) 1 kijiko cha chai
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
(unaweza kuongeza ukipenda)
Chumvi kiasi
Tandoori masala 1 kikubwa cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA .
1. Watoe ngozi na wasafishe vizuri halafu wachuje.
2. Loweka ukwaju na maji kiasi cha kikombe kimoja uvuruge mpake upate urojo mzito, uchuje
3. Tia vitungu saumu na tangawizi vilivyosagwa changanya vizuri na kuku na urojo wa ukwaju.
4. Kisha tia pilipili manga na uzile na chumvi.(chumvi unaweza kuongeza kidogo kwani wakati wa kuchoma kuku watachuja maji hivyo weka ya kutosha).
5. Tia tandoori masala changanya
6. Changanya vizuri na waache wakolee
NAMNA YA KUWACHOMA.
1.
2. Kwenye kifungo cha selector, weka grill na kwenye kifungo cha temperature weka grill vile vile na watachomeka kwa moto wa juu.
3. Waache wachomeke kama dakika 25 hadi 30 hivi, huku watakuwa wanachuja maji na yatakuwa yanadongoka kwenye treya tupu.
4. Wakishakauka na kubadilika rangi vizuri, ondoa treya ya maji yaliyotoka kwenye kuku.
5. Kisha badilisha kifungo cha selector weka bake na kwenye kifungo cha temperature weka 350º weka
6. Kubadilisha vifungo na moto wa kuchomea kunasaidia kuku kuchomeka pande zote mbili bila ya kugeuza geuza.
7. Wakishakauka vizuri watoe, panga kwenye sahani na saladi au pilipili ya kusaga, au chatine. Tayari kwa kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


