Kababu Za Kuchoma Katika Vijiti

Vipimo
Nyama ya kusaga 3 Lb
Thomu 1 kijiko cha chakula
Tangawizi 1 kijiko cha chakula
Chumvi Kiasi
Kotmiri 1 msongo
Bizari ya kababu ½ pakiti ya 100g
(Shan Chapplin Kabaab mix)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Saga nyama pamoja na kotmiri mara mbili iwe laini kuliko ya sambusa.
2. Tia kwenye bakuli na changanya na vitu vyote pamoja.
3. Viringisha kwenye vijiti vya kuchomea na acha
4. Choma (bake) katika oven kwa moto wa 350◦c mpaka zigeuke rangi na kuiva.
5. Zikishaiva ziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa na saladi, chips, mikate au wali.
Kidokezo:
1. Ni bora kuviroweka vijiti vya kuchomea na maji usiku nzima ili ukichoma kababu vijiti visiungue.
2. Tumia bizari zako mwenyewe upendazo ikiwa huna hiyo ya Shan Chapplin Kabaab Mix.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


