Mishkaki Ya Kuku -1

Mishkaki Ya Kuku -1

 

Vipimo:

Kuku kidari (boneless breast) - 4 Ratili (LB)

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Vitunguu - 3

Nyanya - 3

Pilipili boga - 2 

Masala Ya Kuroweka Katika Kuku:

Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Mtindi  - 2 vijiko vya supu

Ndimu - 3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Jiyrah (cummin powder/bizari ya pilau) - 1 kijiko cha supu

Dania (coriander powder/gilgilani) - 1 kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha supu

Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai

Au tumia ukipenda bizari za mishkaki za tayari kama tanduri masala.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Kata kuku vipande vikubwa kubwa kiasi .
  2. Changanya kuku na masala ya vitu vyote katika masala ya kurowekea kuku uroweke kwa muda wa masaa. Katakata vitunguu, nyanya, pilipili boga vipande kiasi.
  3. Tunga vipande vya kuku katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers) huku unatunga baina yake kitunguu, nyanya, pilipili boga.
  4. Tia mafuta kiasi katika kikaango. Mafuta yasiwe mengi hadi yakafunika kuku.
  5. Tumia mafuta kidogo kidogo kila unapoepua kabaab za kwanza ikiwa yamekauka, unaongeza mafuta kidogo kama kiasi ya robo kikombe.
  6. Kaanga kababu za kuku katika moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi kuku awive.
  7. Epua, weka katika sahani ikiwa tayari kuliwa.

Kidokezo:

 Nzuri kuliwa na Hummus na mkate ya kiarabu (pita pan bread) – tazama pishi la Hummus katika Saladi Na Sosi.

  

Share