Skip navigation.
Home kabah

Pweza Wa Kukaanga

    

  

 

Vipimo

 

 

Pweza                                                                   1 Kilo

 

Mafuta                                                                   ½ kikombe

 

Chumvi                                                                  1 kijiko cha chai

 

Tangawizi mbichi iliyosagwa                                    1 kijiko cha chai

 

Thomu iliyosagwa                                                  1 kijiko cha chai

 

Masala ukipenda                                                    1 kijiko cha supu

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 

 

  1. Osha pweza kisha mkatekate  

 

  1. Mtie viungo vyote ulotayarisha  na   chumvi

 

  1. Muache nusu saaa akolee viungo

 

  1. Mtie ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatumbuka maji mwenyewe kwa moto wa kiasi paka awe rangi ya damu yam zee (maroon)

 

  1. Akishawiva kwa rangi hiyo basi sasa mwaga maji yote,chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani

 

  1. Weka karai au kikaango (frying pan) motoni tia mafuta  acha kwa muda wa dakika tano hivi mafuta  yapate moto.

 

  1. Mimina pweza kwenye karai aacha wakaangike paka wabadilike ukiwageuza geuza kila baada ya muda wa dakika kumi hivi.  Pweza tayari kwa kuliwa   kwa ugali au muhogo

 

Kidokezo: 

 

Unaweza kumwagia masala kiasi baada ya kukaanga kama picha inavyo onyesha.