Shurba Ya Nyama Ya Mbuzi Ya Sosi Ya Nyanya

Shurba Ya Nyama Ya Mbuzi Ya Sosi Ya Nyanya

 

Vipimo

 

Nyama ya mbuzi ya mifupa – 1 kilo

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Vitunguu maji (vikate vidogo vidogo) - 2

Nyanya (kata ndogo ndogo)  -  5

Kitunguu saumu (thomu/garlic) – kijiko cha supu

Tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Bizari ya pilau ya unga (Jeera) - 1 kijijo cha chai

Gilgilani ya unga (Dania) - ½  kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga - ¼ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Siki ya zabibu - 3 vijiko vya supu  

Shayiri* /Hariys - 2 vikombe

 

* Shayiri ni aina ya ngano (oats) ila ni tofauti kidogo na ngano. Baadhi ya maduka inajulikana kama ni 'hariys'

 

Kidokezo:

 

Ikiwa shayiri nzima nzima, basi roweka kwa muda wa masaa na uchemshe mpaka ziive.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Weka nyama katika sufuria, tia chumvi, tangawizi, thomu, bizari kidogo, changanya na uweke motoni kidogo ichanganyike na ikolee viungo.
  2. Tia maji, chemsha mpaka iwive.
  3. Katika sufuria nyengine, weka mafuta na kaanga vitunguu kidogo tu vilainike, usiviwache kugeuka rangi.
  4. Tia nyanya, endelea kukaanga, malizia bizari zote.
  5. Mimina sosi ya nyanya katika supu.
  6. Changanya shayiri  na maji katika kibakuli, koroga kisha tia katika shurba.
  7. Iwache ichemke kidogo tu ngano ziwive.
  8. Tia siki na tayari kuliwa. 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

 

Share