Kuku Wa Sosi Tamu (Trinidad)

Vipimo
Kuku 6 LB
Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 vijiko vya supu
Mtindi (Yoghurt) 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha chai
Sosi
Mafuta 2 vijiko vya supu
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Sosi ya tomato (tomato sauce) ¼ kikombe
Sosi ya HP 2 Vijiko vya supu
Cellery 1 mche
Parsley na kotmiri ¼ kikombe
Nyanya 3
Chumvi kiasi
Pilipili manga 1 Kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Mkate kuku vipande vikubwa vikubwa, msafishe kwa siki atoke harufu
2. Mrowanishe na thomu, tangawizi , chumvi, mtindi na pilipili kwa muda wa saa au zaidi.
3. Mtie katika tryea ya kupikia katika oveni.
4. Mchome kwa moto juu (grill) au ukipenda moto wa chini (bake) , akishawiva pakua katika bakuli la kupakulia.
5. Tengeneza sosi kwa kufanya ifuatavyo:
6. Saga kwanza Nyanya, cellery, parsely na kotmiri.
7. Kaaanga thomu katika mafuta kisha tia sosi zote pamoja na mchanganyiko uliosaga wa cellery.
8. Mwagia sosi katika kuku akiwa tayari kuliwa.
Kidokezo : Nzuri kula na wali
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


