Samaki Wa Kupaka Tui La Nazi La Bizari Mchanganyiko

Samaki Wa Kupaka Tui La Nazi Na Bizari Mchanganyiko

Vipimo

Samaki mkubwa wa chango - 1

Tui la nazi zito - 2 vikombe

Pilipili mbuzi -1

Pilipili mbichi kijani -1

Bizari mchanganyiko 1 kijiko cha kulia 

Bizari ya manjano  ½  kijiko cha chai

Ndimu -1 kamua maji

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka tui  katika blender (mashine ya kusagia)  tia vitu vyote isipokuwa ndimu.  
  2. Teka kidogo kisha mroweke samaki kwa mchanganyiko huo wa tui. Kisha muweke katika tray na mchome (grill) katika oven. Akishaiva upande  mmoja mgeuze upande wa pili huku ukimpaka tui.
  3. Tia tui lilobakia katika kisufuria lichemke kidogo tu.
  4. Rojo likianza kuwa zito tia ndimu.
  5. Epua na mwagia juu ya samaki.  Tayari kuliwa.

 

Share