Custard Ya Mdalasini

Custard Ya Mdalasini

VIPIMO
Maziwa -  2 1/2 Vikombe

Mdalasini wa unga - 1 Kijiko cha chai

                           
Mayai -  3

Asali -  1/4 Kikombe 

Chumvi -  Kidogo (dash)

Vanilla - 1 Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Washa oveni moto wa 375F.
  2. Weka vibakuli 6 maalum (remekins) vya kupikia kwenye oven , katika trei ya kuvumbika (bake).
  3. Pasha moto maziwa, mdalasini na vanilla katika sufuria.
  4. Chukuwa bakuli na uchanganye mayai, asali na chumvi pamoja.
  5. Endelea kukoroga, huku unamimina ule mchanganyiko wa maziwakidogo kidogo hadi ichanganyikane vizuri.
  6. Mimina huwo mchanganyiko wa custard kwenye vibakuli ulivyovitayarisha, kisha weka treya
  7. kwenye mlango wa oveni na umimine maji ya moto (yaliyochemka) ili itapakae chini ya vile vibakuli nusu yake.
  8. Pika (bake) katika oven kwa muda wa dakika 30-40 au mpaka ukitovya kisu kitoke kisafi.
  9. Ikisha iiva na kupoa, weka ndani ya friji na ikishapata ubaridiitakuwa tayari kwa kuliwa.

 

 

Share