Kastadi Ya Tambi

Kastadi Ya Tambi

 

Vipimo 

Tambi nyembamba za hudhurungi (brown) -  1/2 pakiti

Maziwa mazito (condensed milk) -  1/2 kikopo

Maziwa ya kawaida -  5 kiasi ya vikombe

Sukari -  1/4 kikombe

Kastadi -  2 vijiko vya supu

Hiliki -  1/4 kijiko cha chai

Zaafarani(roweka katika 1/4 kikombe maji) - 1 kijiko cha chai

Vanilla - 1 kijiko cha chai

Lozi za kukata au njugu za pistachio -  1/2 kikombe  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika: 

  1. Katakata tambi kabisa.
  2. Katika sufuria tia maziwa kisha uchanganye na kastadi ukoroge.
  3. Eka katika moto, tia maziwa mazito (condensed milk), sukari  hiliki, zaafarani na vanilla iache ichemke huku unakoroga bila ya kuachia mkoni ili isifanye madonge.
  4. Ukiona imekuwa nzito ongeza maziwa  mepesi iwe kama kastadi ya kawaida.
  5. Tia tambi uendelee kukoroga usiache mkono, ziache kidogo tu ziive epua na umimine katika bakuli iache ipowe.
  6. Mwagia lozi juu yake.
  7. Tia kwenye friji ikiwa baridi iko tayari.

 

 

Share