Fruti-Saladi

Fruti-Saladi

 

VIPIMO 

Tikiti maji  (water melon) -  1/4

Shammaam (tikiti, cantelope)b-   1/2

Papai -  1

Embe -  1

Peya (pear) -  2

Tofaha (apple) -  2

Machungwa -  2

Plamu (plums) -   3

Pichi (peaches) -  3

Zabibu -  Kiasi

Tango -  1/2

Matunda yoyote mengineyo upendayo -  Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA

  1. Menya papai, katakata vipande vidogo vidogo utie katika chombo cha upendacho cha kupakulia fruit-saladi.
  2. Menya matunda mengine yote yanayohitaji kumenywa na katakata vipande vidogo vidogo kama katika picha.
  3. Katakata tango vipande vidogo vidogo uchanganye.
  4. Unaweza kuongeza sukari kidogo ukipenda.
  5. Wakati wa kupakua katika gilasi katakata ndizi vipande vidogo vidogo ukipenda.
Share