Pudini Ya Mahalabiyyah Na Zaafaraani (UAE)

Pudini Ya Mahalabiyyah Na Zaafaraani (UAE)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo 

 

Unga wa mahindi -6 vijiko cha kulia

Maziwa -3 vikombe

Maziwa mazito (condensed) au malai (cream) -1 kikombe

Sukari -½ kikombe

Maji baridi -1 kikombe

Arki (rose flavour) -½  kijiko cha chai

Zaafaraani -Kijiko cha kulia

Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Weka majani ya zaafaraani katika kikombe cha kahawa utie maji nusu, roweka kidogo.
  2. Weka unga wa mahindi katika kibakuli changanya na maji ya baridi ukoroge.
  3. Weka maziwa katika moto, uchanganye na vitu vyote na uendelee kukoroga katika moto mpaka ichemke vizuri. Ongezea maji ikiwa nzito.
  4. Epua umimine katika vibakuli na pambia lozi au njugu upendazo.
  5. Weka katika friji ipoe ikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share