Boga La Nazi-2

Boga La Nazi 

 

Vipimo: 

Boga - 1

Tui La Nazi -  2  Vikombe

Sukari - 1 kikombe

Hiliki  -  1/2 kijiko cha chai 

 

Namna Ya Kutayarisha na Kupika

 

1.  Unamenya maboga kiasi ukipendacho.

2.  Unayakata kata vipande vidogo vidogo.

3.  Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika.

4.  Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.

5.  Kisha unamimina tui la nazi.

6.  Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.

 

 

Share