Kaimati Za Ndizi

Kaimati Za Ndizi

 

 

Vipimo

Unga - 2 vikombe vya chai

Hamira - 1 kijiko cha chai

Baking powder - 1/2 kijiko cha chai

Sukari - 3 vijiko vya supu

Samli - 1 kijiko cha chai

Yai - 1

Hiliki - 1/4 kijiko cha chai

Maji - 1 1/4 kikombe *

Ndizi mbivu zilizowiva sana - 3

Mafuta ya kukaangia - kiasi

 

* Maji inategemea vikombe, mchanganyiko uwe kama kaimati za kawaida.

 

Namna ya Kutayarisha na Kupika

  1. Katika bakuli, tia unga, hamira, baking powder, sukari, samli, yai na maji.
  2. Changanya vizuri kama kaimati za kawaida.
  3. Katakata ndizi slesi za duara weka kando.
  4. Ukishaumuka chukua slesi ya ndizi uichomve katika unga huku unaifunika ndizi kwa unga wa kaimati. Usiteke unga mwingi bali kidogo tu.
  5. Choma katika mafuta ya moto kama unavyopika kaimati za kawaida.
  6. Eupua chuja mafuta zikiwa tayari.

  

 

 

Share