Vibibi Vya Tui Na Kunyuyuziwa Zabibu

Vibibi Vya Tui Na Kunyuyuziwa Zabibu

 

Vipimo   

 

Mchele vikombe 2

Unga wa ngano 1 kijiko cha kulia

Hamira kijiko 1 cha chai

Tui zito vikombe 2

Maziwa ya unga ¼ kikombe

Hiliki ½  kijiko cha chai

Sukari ½ kikombe

Samli ya kupikia

 

Vipimo Vya Tui La Kupakaza Juu Ya Vibibi

 

Tui zito la nazi 1

Unga wa ngano 1 kijiko cha supu

Sukari ½ kikombe

Maziwa mazito ½ kikombe

Hiliki ½ kijiko cha chai

Arki (rose flavour) ½ kijiko cha chai

Zabibu za kunyunyuzia kiasi

 

Namna Ya Kupika Tui La Vibibi

  1. Changanya vitu vyote katika sufuria ukoroge vizuri kisha weka katika moto huku unakoroga mpaka lichemke kiasi ya dakika chache.
  2. Epua likiwa tayari.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Vibibi

  1. Roweka mchele masaa mengi. Kisha chuja maji
  2. Weka mchele katika mashine ya kusagia (blender) utie tui kidogo kidogo usage mpaka ulainike vizuri.
  3. Tia vitu vilobakia isipokuwa samli usage tena uchanganyike. Kisha mimina katika bakuli uache uumuke.
  4. Weka chuma kidogo katika moto paka samli kiasi ½ kijiko cha chai, teka mchanganyiko umimine katikati.
  5. Kibibi kiwiva chini geuza upike upande wa pili. Endelea upange vibibi katika sahani.
  6. Pakaza tui lake na nunyizia zabibu. Tayari kuliwa.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share