Nia Ya Swawm Ni Kwa Kila Siku Au Mara Moja Inatosha
SWALI:
kuna nukta chache ningependa ufafanuzi zaidi.
Kuhusu nia, nimetatizika kidogo maana masheikh wetu huku wanatuambia inabidi kunuia kila siku. Na
Naomba ufafanuzi, usahihi ni vipi kuhusu nia, ukitia nia siku ya kwanza yatosha kufunga mwezi mzima ama lazima kila siku unuie
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Hakika ni kuwa hili ni suala sahali lakini kwa sababu ya kutaka kuongeza mambo katika Dini yetu tunawapatia ugumu Waislamu wa kawaida bila ya kuwa na haja aina yoyote.
Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) hata kwa mwezi wa Ramadhaan Anatutakia usahali pale Aliposema:
“Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi atayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Allaah Anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Allaah kwa kuwa Amekuongoeni ili mpate kushukuru” (2: 185).
Na katika hali zote Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema: “Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini” (22: 78).
Sheria za Kiislamu zimekuja kuhafifisha na kuondoa uzito mwingi uliokuwepo.
Ya kustaajabisha ni kuwa utapata katika mambo mengi tunarudisha ugumu usiokuwepo. Mfano ni mas-ala nia katika Funga ya Faradhi, kulipa Funga ya Faradhi au Kafara. Katika Swawm zote hizo ni lazima Muislamu atie nia na bila nia mfungaji hatakuwa na Swawm.
Lakini je, nia inatiwa namna gani? Utapata katika sehemu nyingi ulimwengu watu wanatilishwa nia na ima Imaam au Mwadhini au Shaykh ilhali jambo
Hakika kuhusu nia ni kuwa inafaa itiwe katika sehemu yoyote ya usiku hata ikiwa ni sekunde chache kabla ya Alfajiri ya kweli (yaani wakati wa adhana ya pili). Maana ya nia hasa ni kuazimia kwa moyo kutekeleza amali Fulani, na kuitamka kwa ulimi ni uzushi usiofaa katika Dini. Mfungaji katika mwezi wa Ramadhaan inamtosha kutia nia ya kufunga mwezi mzima pindi mwezi huo unapoingia.
Na hata
Suala ni kuwa huwa tunafanya hivyo kwa ajili gani? Sababu kuu ni kufunga siku ya pili, na kufanya hivyo tayari huwa umetia nia kwa ajili ya Funga ya siku hiyo ya pili. Hata kama hukuweza kuinuka kwa sababu moja au nyingine huwa umetia nia na Swawm yako ni sawa.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
