Viungo Vya Mwili Vitashuhudia Matendo Ya Mwana-Aadam Siku Ya Qiyaamah

 

 

Viungo Vya Mwili Vitashuhudia Matendo

Ya Mwana-Aadam Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa): 

 

الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٦٥﴾

 Leo Tunatia vizibo juu ya vinywa vyao, na itatusemesha mikono yao, na itashuhudia miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.[Yaasiyn: 65]

 

 

Siku ya Qiyaamah viungo vya miili vitakuwa ni vyenye kushuhudia matendo ya bin-Aadam aliyoyatenda hapa duniani: Mfano mikono itasema: "Niliiba kadhaa wa kadhaa".  Miguu itasema: "Nilikwenda sehemu za maasi." Macho yatasema:  "Nilitazama machafu." Masikio yatasema: "Nilisikiliza nyimbo, au umbea au ghiybah (kusengenya)." Na mengineyo kadhaalika.

 

 

Na hivi ndivyo itakavyokuwa hali ya makafiri, wanafiki na wenye kumuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Siku ya kufufuliwa, watakapokanusha madhambi waliyoyatenda duniani na kuapa kwamba hawakuyafanya. Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Atawafunga midomo yao kisha Ataviamrisha viungo vizungumze kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

 

 عن أنس بن مالك قال: كنا عند النبي صلى الله عليه وسلم، فضحك حتى بدت نواجذه، ثم قال:  ((أتدرون مم أضحك؟)) قلنا: الله ورسوله أعلم. قال: ((من مجادلة العبد ربه يوم القيامة، يقول: رب : ألم تجرني من الظلم؟ فيقول: بلى. فيقول: لا أجيز علي إلا شاهدًا من نفسي.   فيقول كَفَى بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ  ، وبالكرام الكاتبين  شهودا. فيختم على فيه، ويُقال لأركانه: انطقي. فتنطق بعمله، ثم يخلى بينه وبين الكلام، فيقول: بُعدًا لَكُنَّ وسُحقًا، فعنكنَّ كنتُ أناضل))  مسلم والنسائي

 

Imetoka kwa Anas Bin Maalik ambaye alisema, Tulikuwa na Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akacheka mpaka magego yake yakaonekana, kisha akauliza: “Je? Mnajua kwa nini nacheka?” Tukasema: Allaah na Rasuli wake Wanajua.  Akasema: “(Nacheka) kwa sababu ya majadiliano wa mja na Rabb wake Siku ya Qiyaamah, atasema: Ee Rabb wangu, hutonihifadhi na dhulma? (Allaah) Atasema: Bila shaka. Atasema:  Sitokubali  shahidi yeyote dhidi yangu isipokuwa  mwenyewe. (Allaah) Atasema:  Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu. Na watukufu wenye kuandika watakuwa mashahidi dhidi yako.  Kisha mdomo wake utazibwa na vitaambiwa viungo vyake: Sema! (Viungo) vitasema aliyoyafanya. Kisha ataachiwa aseme na atasema (kuviambia viungo vyake): Angamieni, kwani ilikuwa kwa ajili yenu nikigombania.”   [Muslim 4.2280 na An-Nasai  katika Al-Kubrah 6:508]

 

 

Hadiyth nyingine:

 

 عن أبو موسى الأشعري، رضي الله عنه: ((يُدعى المؤمن للحساب يوم القيامة، فَيَعْرضُ عليه رَبُّه عملَه فيما بينه وبينه، فيعترف فيقول: نعم أيْ رب، عملتُ عملتُ عملت. قال: فيغفر الله له ذنوبه، ويستره منها. قال: فما على الأرض خَليقة ترى من تلك الذنوب شيئًا، وتبدو حسناته، فَوَدَّ أن الناس كلهم يرونها، ويُدعى الكافر والمنافق للحساب، فَيَعرضُ رَبُّه عليه عمله، فيجحد وفيقول: أي رب، وعزتك لقد كتب علي هذا الملك ما لم أعمل. فيقول له الملك: أما عملت كذا، في يوم كذا، في مكان كذا؟ فيقول: لا وعزتك أيْ رب ما عملتُه. فإذا فعل ذلك خُتِم على فيه((. قال أبو موسى الأشعري: فإني أحسب أول ما ينطق منه الفخذ اليمنى، ثم تلا  الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٦٥﴾

Imetoka kwa Abu Musa Al-Ash'ariyyi (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  kwamba: Muumini ataitwa kuhesabiwa siku ya Qiyaamah, na Rabb wake atamuonyesha amali zake,  baina yake na Rabb wake Atakubali na kukiri kwa kusema: Ndio Rabbi, nimefanya hayo.  Kisha Allaah Atamghufuria madhambi yake na kuyaficha wala hakuna kiumbe katika ardhi atakayeona madhambi hayo, lakini vitendo vyake vyema vitaonekana na Atataka watu wote wavione. Kisha Kafiri na Munaafiq ataletwa hesabuni na Rabb wake Atamuonyesha vitendo na atakanusha kwa kusema: Ee Rabb kwa Utukufu Wako, Malaika huyu ameandika vitendo ambavyo sikuvifanya. Malaika atasema kumwambia: Hukufanya kadha na kadhaa, siku kadhaa na kadhaa? Atasema: Kwa Utukufu wako sikufanya.  Atakaposema hivi, Allaah Atamziba mdomo wake.” Abu Musa Al-Ash'ariyyi (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kasema: nafikiri kiungo cha kwanza kuzungumza kitakuwa ni paja la kulia. [Imaam Ahmad] Kisha akasoma:

 

الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٦٥﴾

Leo Tunatia vizibo juu ya vinywa vyao, na itatusemesha mikono yao, na itashuhudia miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.” [Yaasiyn: 65]

 

 

Hivyo ndivyo viungo vya mwili vitakavyomchongea mtu muovu siku ya Qiyaama kwa vitendo viovu vyote alivyovitenda. Na ushahidi mwingine ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Kauli Zake:   

 

 

وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّـهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ﴿١٩﴾حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٠﴾وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّـهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٢١﴾وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾ 

 

Na Siku watakayokusanywa maadui wa Allaah kwenye moto, nao watakusanywa kupangwa safusafu. Mpaka watakapoufikia yatashuhudia dhidi yao, masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. Na wataziambia ngozi zao: Mbona mnashuhudia dhidi yetu? Zitasema: Ametutamkisha Allaah Ambaye Ametamkisha kila kitu, Naye Ndiye Aliyekuumbeni mara ya kwanza na Kwake mtarejeshwa. Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu, na wala ngozi zenu; lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda. [Fusw-Swilat: 19-22]

 

 

 

Na pia kama Anavyosema Allaah ('Azza wa Jalla) kwamba Siku hiyo hakuna mtu atakayeweza kukanusha matendo yake maovu kwa sababu amali zinarekodiwa na hakuna kinachokosekana kurekodiwa hata chembe: 

 

وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا ﴿١٣﴾ اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا ﴿١٤﴾

Na kila bin Aadam Tumemuambatanishia majaaliwa ya ‘amali zake shingoni mwake. Na Tutamtolea Siku ya Qiyaamah kitabu akutane nacho kimekunjuliwa. (Ataambiwa): Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosheleza leo kukuhesabu. [Al-Israa: 13- 14]

 

 

Na Anasema pia Allaah ('Azza wa Jalla):

 

وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ ﴿٤٧﴾

Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah; basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote. Na japo ikiwa uzito wa mbegu ya haradali, Tutaileta. Na inatosheleza Kwetu kuwa Wenye kuhesabu. [Al-Anbiyaa: 47]

 

 

Na pia:

 

يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾ فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

Siku hiyo watatoka watu makundi mbalimbali wamefarikiana ili waonyeshwe ‘amali zao. Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona.

Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (au sisimizi) ataiona. [Al-Zalzalah: 6 – 8]

 

 

Kwa hivyo inampasa Mwana-Aadam ajichunge na maovu na atambue kuwa viungo alivyoumbwa navyo katika mwili wake ni kwa ajili ya matumizi yenye kumridhisha Rabb wake, na sio kwa ajili ya maasi, kwani kila kiungo kitakuja kuulizwa kama Anavyosema Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

 …   إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾ 

“Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitaulizwa.” [Al-Israa: 36]

 

Inamaanisha: Mtu ataulizwa siku ya Qiyaama kuhusu hivyo viungo (alivyovitumia) na viungo vitaulizwa kuhusu yeye (Mtu) na ataulizwa kavitumia vipi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

 

Share